KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anategemea wachezaji wake wote kuonyesha kujivunia kuiwakilisha nchi yao kwa kuimba wimbo wa taifa katika michuano ya Kombe la Dunia. Hodgson anataka kikosi chake kuonyesha uzalendo wakati wimbo wao wa taifa uitwao God Save The Queen utakapokuwa ukipigwa katika mechi zao nchini Brazil. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66 aliendelea kudai tayari ameshazungumza na wachezaji wake kuhusiana na hilo na anategemea wataonyesha umoja wao kwa kuimba wimbo huo kwa sauti katika mechi zao. Uingereza tayari wameshatua jijini Miami, Marekani kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Italia unatarajiwa kuchezwa Juni 14 huko Manaus. Kabla ya kuelekea Brazil wanatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Ecuador Jumatano na Honduras Jumamosi inayokuja.
No comments:
Post a Comment