Tuesday, July 8, 2014

ADIDAS YADAI KUFUATILIA KWA KARIBU MGOGORO WA NFF.

KAMPUNI ya vifaa vya michezo kutoka nchini Ujerumani ya Adidas, imedai kuwa mkataba wake na Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF hautakuwa na mabadiliko yoyote lakini watakuwa wakifuatilia kwa karibu mgogoro uliolikumba shirikisho hilo katika siku za karibuni. Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na taarifa zilizozagaa kuwa kampuni hiyo imesimamisha udhamini wake na NFF kutokana na sakata la kusimamishwa viongozi wake na mahakama moja nchini humo. Meneja mawasiliano wa Adidas, Lars Mangels alifafanua kuwa hawajabadilisha chochote katika mkataba wao na NFF lakini wanafuatilia hali ya mambo inavyoendelea katika shirikisho hilo. Toka timu ya taifa ya Nigeria iondolewa katika hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil, kumekuw ana migogoro iliyoikumba NFF mpaka kufikia hatua ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutishia kuifungia nchi hiyo kama serikali itaendelea kuingilia mambo ya soka. Mahakama moja ya mji wa Jos ilitoa amri kwa viongozi wote wa kamati ya utendaji ya NFF kuachia madaraka hatua ambayo ni kinyume na sheria za FIFA.

No comments:

Post a Comment