Monday, July 7, 2014

ASHLEY COLE ATUA RASMI ROMA.

KLABU ya AS Roma ya Italia imethibitisha kumsajili beki Ashley Cole kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kuondoka katika klabu ya Chelsea. Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza amepewa mkataba huyo ambao utakuwa na thamani ya euro milioni 2.5 kwa mwaka hivyo kumaanisha kuwa atakuwa akilipwa kiasi cha euro 48,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi. Taarifa za kusajiliwa kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 33 zilizothibitishwa kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter wa mchezaji huyo. Cole alipewa mkataba mpya na Chelsea ambao ulikuwa na punguzo la mshahara wake lakini alikataa na kuamua kutafuta changamoto mpya kufuatia kustaafu rasmi soka la kimataifa. Cole amefanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza mara tatu ambapo mara mbili ameshinda akiwa na Arsenal na mara moja akiwa na Chelsea na pia mataji saba ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment