Wednesday, August 20, 2014

GUINEA YAHAMISHIA MCHEZO WAKE NA TOGO CASABLANCA KUKIMBIA EBOLA.

KUFUATIA uamuzi wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kusimamisha nchi zote zilizoathirika na Ebola kutumia viwanja vyao vya nyumbani kwa ajili ya mechi za kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika, Guinea imetangaza kucheza na Togo jijini Casablanca, Morocco. Ugonjwa wa Ebola ulilipuka Guinea kuanzia Januar na kusambaa katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Nigeria na kuuwa watu zaidi wa 1,229 kwamujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani-WHO. Togo walilalamika CAF mapema mwezi huu kuhusu hatari ya kusafiri kwenda katika mji mkuu wa Guinea, Conakry kucheza dhidi ya wenyeji wao hao. Mchezo huo wa ufunguzi wa kundi E unatarajiwa kuchezwa Septemba 5 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment