Monday, September 1, 2014

KOSCIELNY ATOLEWA KATIKA KIKOSI CHA UFARANSA KUFUATIA MAUMIVU YA KICHWA.

BEKI wa klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny amelazimika kujitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kupata majeraha ya kichwa. Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 aligongana kwa vichwa na Jeffrey Schlupp mapema katika mchezo ambao Arsenal iliambulia sare ya 1-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa jana. Muda mchache mara baada ya tukio hilo Koscielny alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Clalum Chambers katika dakika ya 26 ya mchezo. Shirikisho la Soka la Ufaransa sasa limethibitisha kuwa majeruhi hayo yatamfanya kukosa mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Hispania na Serbia. Nafasi yake itachukuliwa na beki mpya aliyesajiliwa na Barcelona akitokea Valencia Jeremy Mathieu .

No comments:

Post a Comment