Tuesday, January 6, 2015

PODOLSKI AKAMILISHA MKOPO WAKE INTER MILAN.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Lukas Podolski amekamilisha rasmi uhamisho wake wa mkopo kutoka klabu ya Arsenal kwenda Inter Milan jana. Wakati Podolski akiwa jijini Milan toka wiki iliyopita, Inter wametangaza jana kuwa taratibu zote za uhamisho wa mchezaji mpaka Juni mwaka huu zimekamilika. Kuna uwezekano mkubwa wa Podolski kujumuishwa katika kikosi cha Inter ambacho kitawavaa vinara wa Serie A Juventus baadae leo. Ujio wa Podolski Inter itakuwa ahueni kubwa kwa kocha Roberto Mancini ambaye alikuwa anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. Podolski mwenye umri wa miaka 29 amefunga mabao 47 katika mechi 121 alizoichezea Ujerumani ingawa ameshindwa kung’ara akiwa Arsenal katika siku za karibuni kwa kushindwa kufunga katika mechi sita za ligi alizocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment