KATIKA tetesi za usajili klabu ya Chelsea inajiandaa kutenga kitita cha paundi milioni 200 kwa ajili ya kutengua mkataba na kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Katika siku za karibuni kumekuwa na tetesi kutoka vyombo vya habari nchini Hispania kuwa Messi hana furaha Barcelona toka Luis Enrique ateuliwe kuwa kocha, ingawa habari hizo zimepingwa vikali na rais wake aliyedai mchezaji huyo ana furaha na hataondoka. Kwa upande mwingine Liverpool nao wanataka kumsajili beki wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Manchester City James Milner mwenye umri wa miaka 29 ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Gazeti la Daily Stars nalo limeripoti kuwa Manchester United wametoa ofa kwa ajili ya beki wa kati wa kimataifa wa Ujerumani Mats Hummels pamoja na klabu yake ya Borussia Dortmund kuweka ngumu kuwa haitamuuza beki huyo. Winga mahiri wa kimataifa wa Uingereza Andros Townsend mwenye umri wa miaka 23 amesisitiza kuwa anataka kuendelea kubakia Tottenham Hotspurs kwa kipindi kirefu kijacho pamoja na kuhusishwa na tetesi za kuondoka. Klabu ya Arsenal wametupiwa ofa yao ya paundi milioni tano na klabu ya Dinamo Zagreb kwa ajili ya kumsajili kiungo Marcelo Brozovic. Klabu za Everton, Liverpool, Tottenham Hotspurs na Valencia nazo zinaonekana kumfukuzia nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.

No comments:
Post a Comment