Thursday, June 11, 2015

IBRAHIMOVIC APIGIWA CHAPUO KWENDA AC MILAN.

MTOTO wa kiume wa rais wa AC Milan, Silvio Berlusconi anaamini Zlatan Inrahimovic anaweza kuisaidia klabu hiyo kama akiamua kurejea majira haya ya kiangazi. Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 33 aliondoka Milan kwenda Paris Saint-Germain kiangazi mwaka 2012 kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa ikiuza wachezaji wake nyota ili kukabiliana na mtikisiko wa uchumi. Toka wakati huo, Ibrahimovic amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu Ufaransa wakati Milan wakimaliza katika nafasi ya nane na 10 katika Serie A katika misimu miwili toka aondoke. Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Sweden ameingia katika miezi yake 12 ya mwisho katika mkataba wake PSG na amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea tena San Siro. Mtoto wa bilionea huyo, Piero Berlusconi amesema siku zote amekuwa akimhusudu Ibrahimovic na anadhani anaweza kuisadia Milan kwa kiasi kikubwa kama akirudi.

No comments:

Post a Comment