MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Al Ahly ya Misri wamefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kea ushindi wa matuta dhidi ya Club Africain ya Tunisia. Club Africain walifanikiwa kushinda mchezo huo wa maruadiano wa mtoano kea mabao 2-1 na kugeuza matokeo kuwa sare ya mabao 3-3 baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Sare hiyo ilipelekea mchezo huo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Al Ahly waliibuka kidedea kea kufunga penati 5-4. Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo, CS Sfaxien wao walikuwa na bahati kuliko wa Tunisia wenzao baada ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast. Katika michezo mingine Etoile du Sahel walifanikiwa kugeuza matokeo ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza na kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa meridian dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na kuifanya kuwa timu ya tatu kutoka Tunisia kuingia hatua ya makundi. Mabingwa wa zamani wa Afrika Zamalek ya Misri pia nao walifanikiwa kugeuza matokeo ya kufungwa mechi ya mkondo wa kwanza na kushinda mabao 3-1 nchini Misri dhidi ya Sanga Balende ya DR Congo hivyo kusonga mbele lwa jumla ya mabao 3-2. Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini wao waliingia hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuitabdika AS Kaloum ya Guinea kea mabao 4-1 katika mchezo wa maruadiano uliofanyika Soweto hivyo kusonga mbele kea jumla ya mabao 6-1.
No comments:
Post a Comment