Monday, December 14, 2015

CHAMPIONS LEAGUE DRAW: ARSENAL KUVAANA NA BARCELONA, PSG NA CHELSEA TENA.

MABINGWA watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Barcelona wamepangwa kucheza na Arsenal katika hatua ya timu 16 bora ikiwa imepita miaka 10 toka timu hizo kukwaana katika hatua ya fainali. Chelsea na Paris Saint-Germain-PSG nao wanatarajiwa kukutana kwa mara nyingine tena baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kung’olewa na vijana wa Jose Mourinho katika hatua hiyo msimu uliopita. Mechi nyingine itakayokutanisha vigogo ni mabingwa wa Italia Juventus watakaowavaa mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich, wakati bingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid yeye atacheza dhidi ya AS Roma. PSV Eindhoven wao watakwaana na Atletico Madrid, Dinamo Kiev dhidi ya Manchester City na Benfica wataivaa Zenit Saint Petersburg. Gent ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza wao wamepangwa kucheza na Wolfsburg ya Ujerumani. Mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa Februari 16-17 na 23-24 huku zile za marudiano zikitarajiwa kuchezwa Machi 8-9 na machi 15-16.

No comments:

Post a Comment