MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amedai mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy ana ubora unaoweza kumpa mafanikio katika klabu kubwa. Vardy ametawala Ligi Kuu msimu huu, akiwa amefunga mabao 14 na kuweka rekodi mpya ya kufuga mabao 11 katika mechi 11 mfululizo. Mourinho amesema nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28, anaweza kufanikiwa popote. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Vardy ni mfungaji bora hivyo ni kawaida kwa klabu kubwa kumuwinda. Chelsea wanatarajiwa kuwa wageni wa Leicester City Jumatatu katika mchezo wa ligi utakaofanyika katika Uwanja wa King Power.

No comments:
Post a Comment