Wednesday, December 9, 2015

PIGO BARCELONA, NEYMAR AUMIA MAZOEZINI.

MABINGWA wa Ulaya, Barcelona wamepata pigo kufuatia nyota wake wa kimataifa wa Brazil, Neymar kuumia mazoezini jana wakati wakijiandaa na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen. Katika taarifa ya klabu iliyotumwa katika mtandao ilithibitisha taarifa hizo na kuongeza kuwa nyota huyo atafanyiwa vipimo ili kubaini ukubwa wa tatizo lake. Neymar mwenye umri wa miaka 23, anategemewa kuka nje katika mchezo dhidi ya Leverkusen, lakini kuna wasi wasi kwa Barcelona kama ataweza kupona kwa wakati kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ambapo timu hiyo imepangwa kucheza hatua ya nusu fainali Desemba 17 mwaka huu. Barcelona watamaliza wakiwa vinara wa kundi E hata wakipata matokeo yeyote yale, lakini meneja Luis Enrique amesisitiza kuwa watakwenda katika mchezo huo kutafuta ushindi.

No comments:

Post a Comment