NAHODHA wa Manchester United Wayne Rooney anaweza kurejea tena uwanjani kesho katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Norwich City. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye kama akicheza mchezo huo atakuwa ametimiza mechi 500 akiwa mchezaji wa United, alikosa michezo mitatu iliyopita kwasababu ya majeruhi ya kifundo cha mguu. Meneja wa United Louis van Gaal amebainisha kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akifanya mazoezi wiki yote hii. Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 amesema anaweza kucheza lakini inabidi kusubiri na kuona kama itawezekana.
No comments:
Post a Comment