Sunday, December 13, 2015

SINA MPANGO WA KUINOA MAN UNITED - NEVILLE.

NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amebainisha kuwa haoni kama ataweza kuja kuifundisha klabu hiyo siku za usoni. Neville mwenye umri wa miaka 40, ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa Valencia mapema mwezi huu, aliibukia katika shule ya United na baadae kuitumikia kwa miaka 19. Lakini pamoja na kupita hatua moja katika kibarua chake kipya cha ukocha, beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza haoni kama anaweza kurejea Old Trafford siku zijazo na anachozingatia sasa ni kuisaidia timu yake kukua. Neville amesema anafahamu anachohitaji katika maisha yake na suala la kuinoa United siku zijazo halipo mawazoni mwake.

No comments:

Post a Comment