MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa jambo moja kuwa linalompa nguvu ya kusonga mbele kwa kipindi kirefu katika shughuli zake za ukocha ni muziki wa Bob Marley. Wenger ni shabiki wa kutupwa wa mwanamuzi huyo wa rege wa Jamaica ambaye kazi zake hupenda kuzisikiliza mara nyingi pindi akiendesha kuelekea katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo. Akihojiwa na gazeti moja la Ufaransa, Wenger alikiri kumhusudu Bob Marley kwasababu alikuwa sio mzushi bali mkweli nay eye huwapenda watu wa aina hiyo. Arsenal itajitupa uwanjani kesho kukwana na Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu huku pia wakikabiliwa na mchezo wa kufa na kupona wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiakos jijini Athens Jumatano ijayo.
No comments:
Post a Comment