Monday, December 7, 2015

ZIDANE AMKINGIA KIFUA BENZEMA.

NGULI zamani wa soka wa Ufaransa, Zinedine Zidane hataki kuona Karim Benzema aliondolewa katika kikosi cha nchi hiyo kutokana na nyota huyo kudaiwa kuhusika katika kashfa ya mkanda wa ngono unaomhusu Mathieu Valbuena. Benzema anakabiliwa na mashitaka ya kushirikiana na wasaliti katika sakata hilo na rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa-FFF Noel Le Graet ameitisha mkutano na wana habari Alhamisi hii kuzungumzia suala hilo. Kuna taarifa zinadai kuwa uamuzi utakaochukuliwa ni kumsimamisha Benzema kuitumikia nchi hiyo mpaka hapo uchunguzi dhidi yake utakapokamilika na kutolewa matokeo yake. Hata hivyo, Zidane ana matumaini Benzema ataruhusiwa kuendelea kuitumikia nchi hiyo kwani anahitaji kikosi chao kiwe imara ili kiweze kuwa na nafasi ya kunyakuwa michuano ya Ulaya mwakani ambayo itafanyika katika ardhi yao. Akihojiwa Zidane amesema inabidi wasubiri mpaka Alhamisi lakini kwa mawazo yake anadhani jambo jema kwa nchi hiyo na mchezaji ni kumuepusha na adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment