Monday, January 18, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich Robert Lewandowski ameripotiwa kutofurahia kuwepo hapo baada ya nafasi ya Pep Guardiola kuchukuliwa na Carlo Ancelotti na anataka kujiunga na Paris Saint-Germain majira ya kiangazi.
Chanzo: Fechajes.net

KLABU ya Liverpool imejiunga katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, wakati Mario Balotelli anaweza kujiunga na West Ham United. Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anadaiwa kutofurahishwa na kiwango cha Balotelli ndio maana anataka kumrejesha Hernandez Uingereza.
Chanzo: Don Balon

KLABU ya Borussia Dortmund inajipanga kumuwania kiungo wa Chelsea Ramires katika majira ya kiangazi ili kuziba nafasi ya Ilkay Gundogan ambaye anataka kwenda Juventus.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU ya Chelsea imemuweka mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette katika mipango yao ya usajili wa majira ya kiangazi kama Eden Hazard ataondoka Stamford Bridge.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU ya Real Madrid inajipanga kufanya usajili wake wa kwanza kipindi hiki cha Januari kwa kumtengea euro milioni 15 kiungo wa klabu ya Boca Juniors Rodrigo Betancur, ingawa bado ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa mkopo.
Chanzo: Sport

NYOTA wa Liverpool, Jerome Sinclair anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi baada ya kushindwa kuafikiana juu ya mkataba mpya.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment