Tuesday, March 15, 2016

BENITEZ AJIPA MOYO NA KIKOSI CHAKE.

MENEJA mpya wa Newcastle United, Rafa Benitez amesema timu hiyo imeonyesha dalili chanya pamoja na kipigo cha bao 1-0 walichopata kutoka kwa Leicester City jana na kusisitiza wanaweza kuepuka kushuka daraja. Newcastle bado imeendelea kubakia katika eneo la kushuka daraja baada ya kupoteza mchezo wa kwanza toka Benitez raia wa Hispania ateuliwe. Klabu hiyo imebakiza michezo tisa huku mmojawapo utakaofuata ukiwa dhidi ya Sunderland ambao nao wanapigana wasishuke daraja. Benitez ambaye alichukua mikoba ya Steve McClaren aliyetimuliwa Ijumaa iliyopita amesema anaamini kwa juhudi zilizoonyeshwa na kikosi chake wanaweza kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment