Thursday, March 3, 2016

KAMARA ASAINI MKATABA MPYA MLS.

KLABU ya Columbus Crew inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS, imethibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Sierra Leone Kei Kamara amesaini mkataba. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 31 amesaini mkataba mwingine ambao utamuweka katika klabu hiyo yenye maskani yake huko Ohio mpaka mwaka 2018. Mkurugenzi wa michezo na kocha wa klabu hiyo, Gregg Berhalter alithibitisha taarifa hizo na kudai kujivunia kuendelea kuwa na Kamara katika kikosi chao. Kocha huyo amesema kwa upande wake Kamara ni ushahidi tosha wa historia ya mafanikio katika ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment