MSHAMBULIAJI wa zamani wa Uholanzi, Patrick Kluivert amedai Newcastle United wana wachezaji wakubwa hivyo kuna uwezekano mkuba wa kubakia katika Ligi Kuu kufuatia ujio wa meneja mpya Rafa Benitez. Benitez aliyetimuliwa Real Madrid Januari mwaka huu, alichukua mikoba kutoka Steve McClaren Ijumaa iliyopita na kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Leicester City. Newcastle wanashikilia nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi huku wakiwa wamebaki na mechi tisa kuhakikisha wanabakia katika Ligi Kuu. Kluivert ambaye aliwahi kuichezea Newcastle kati ya mwaka 2004 na 2005 ana uhakika kuwa Benitez atafanya kila awezalo kuhakikisha wanabaki juu. Akihojiwa Kluivert amesema Benitez ni kocha mzuri na ameonyesha hilo kwa klabu kadhaa ndio maana ana uhakika kuwa anaweza kuipeleka mbele klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment