Tuesday, March 15, 2016

MBIO ZA UBINGWA BADO ZIKO WAZI.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesisitiza mbio za taji la Ligi Kuu hazijabaki kwa timu yake pekee na Tottenham Hotspurs. Leicester wako kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tano huku wakiwa wamebaki na mechi nane baada ya kuichapa Newcastle United bao 1-0 jana. Spurs wao wako nafasi ya pili, huku Arsenal wakiwa nyuma ya vinara hao kwa alama 11 na Manchester City wako nafasi ya nne wakiwa nyuma kwa alama 12. Akihojiwa kama anadhani Leicester au Spurs ndio wanaweza kuwa mabingwa, Ranieri mwenye umri wa miaka 64 amesema mbio za ubingwa bado ziko wazi ingawa kuna watu wengi wameshaaza kuota. Ranieri amesema jambo muhimu analofikiria yeye ni kupata ushindi katika mchezo ulio mbele yao hivyo anaamini bado wana kazi ngumu mbele yao.

No comments:

Post a Comment