NAHODHA wa zamani wa Brazil na beki wa AS Roma, Cafu anaamini winga wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah atakuwa mwiba mchungu kwa Real Madrid wakati klabu hizo mbili zitakapokutana. Kauli ya nguli huyo wa soka imekuja akizungumzia mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao utazikutanisha timu hizo. Cafu amesema bado mpaka sasa hawafahamu nani atacheza katika mechi hiyo lakini ni kweli Salah anawea sababisha madhara kwa Madrid ingawa watahitaji kucheza kitimu zaidi. Mchezo huo wa maruadiano unatarajiwa kufanyika Santiago Bernabeu Machi 8 mwaka huu na Madrid tayari wako mbele kwa mabao 3-0 waliyopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Italia.
No comments:
Post a Comment