Friday, March 18, 2016

VAN GAAL AIGEUKIA CITY BAADA YA KUTOLEWA EUROPA LEAGUE.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema lazima waifunge Manchester City ili kuweka matumaini yao hai ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. United waling’olewa katika michuano ya Europa League na Liverpool jana na mchezo wao unaofuata ni dhidi ya City ambao wanashika nafasi ya nne huku wakiwa alama nne mbele yao katika msimamo wa Ligi Kuu. Akihojiwa Van Gaal amesema ni lazima waifunge City kwasababu ndio nafasi pekee ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anafahamu watu wanategemea makubwa lakini haina shaka kwani wanaweza kupambana na shinikizo hilo.

No comments:

Post a Comment