Friday, April 1, 2016

BARCELONA KUMUENZI CRUYFF.

KLABU ya Barcelona inatarajia kutoa heshima yake kwa mchezaji na kocha wa zamani nguli Johan Cruyff wakati watakapokwaana na mahasimu wao Real Madrid katika Clasico kesho. Mchezaji ambao hutazamwa zaidi duniani ni wa kwanza kwa Barcelona toka Cruyff alipofariki dunia kwa saratani akiwa na umri wa miaka 68 wiki iliyopita. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo mashabiki zaidi ya 90,000 watakaojitokeza katika Uwanja wa Camp Nou wataonyesha ujumbe wa kumshukuru nguli huyo huku wachezaji nao wakivaa fulana zenye ujumbe kama huo. Nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta amesema kutokana na umuhimu wa mchezo huo watajitahidi kadri ya uwezo wao kushinda mchezo huo kwa heshima ya Cruyff. Barcelona ambao wanaongoza La Liga kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Madrid, walishinda mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba mwaka jana kwa mabao 4-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

No comments:

Post a Comment