Friday, April 1, 2016

FENERBAHCE KUMUWANIA SCHWEINSTEIGER KIANGAZI.

KLABU ya Fenerbahce inadaiwa kujipanga kumuwani kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshindwa kuonyesha makeke yake katika msimu wake wa kwanza Old Trafford suala ambalo limechangiwa na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara. Kufuatia kuwanasa Nani na Robin van Persie katika kikosi chao msimu uliopita, klabu hiyo ya Uturuki imepania kwa mara nyingine kumwaga fedha katika kipindi cha usajili kwa ajili ya kujiimarisha na msimu ujao. Kiungo huyo wa zamani wa Bayern Munich anadaiwa kuwa anaweza kununuliwa kwa euro milioni saba kama Fenerbahce wakiamua kumchukua.

No comments:

Post a Comment