MENEJA wa Arseal, Arsene Wenger alikuwa akitegemea kuwepo maandamano makubwa zaidi wakati wa mchezo walioshinda bao 1-0 dhidi ya Norwich City Jumamos iliyopita. Wenger anatarajiwa kutimiza mwaka wa 20 akiiongoza Arsenal itakapofika Octoba mwaka huu, lakini mara ya mwisho kutwaa taji la Ligi Kuu ilikuwa mwaka 2004 na baadhi ya mashabiki walishikilia mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kutaka mabadiliko katika Uwanja wa Emirates. Akihojiwa Wenger amesema alitegemea uwanja mzima kuwa rangi nyeupe za mabango ya waandamanaji katika mchezo huo. Meneja huyo aliongeza kuwa lengo lilikuwa ni kuwapa furaha mashabiki hao kwa asilimia 100 lakini kwa bahati mbaya ameshindwa kutimiza hilo. Ushindi huo umefanya Arsenal kukwea katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ambapo sasa wanahitaji alama mbili pekee ili wakihakikishie nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Jumapili hii Arsenal watakuwa na kibarua kizito pale watakaposafiri kuifuata Manchester City katika mchezo wa ligi utakaofanyika Uwanja wa Etihad.
No comments:
Post a Comment