KLABU ya Chelsea imethibitisha kuondoka kwa wachezaji waliosajili kwa mkopo Alexandre Pato, Radamel Falcao pamoja na kipa wa akiba Marco Amelia. Makubaliano ya mkopo kwa Paton a Falcao yalimalizika jana huku Amelia akiwa mchezaji huru kufuatia kusaini mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo Octoba mwaka jana ili kumsaidia kipa namba moja Thibaut Courtois ambaye alikaa nje kwa miezi mitatu msimu uliopita kutokana na majeruhi ya goti. Klabu ilitangaza taarifa za kuwaacha wachezaji hao katika mtandao wake na kuwashukuru kwa mchango wao katika kipindi chote walichokuwa nao huku wakiwatakia mafanikio popote watakapokwenda. Mapema wiki hii, wakala wa Pato, Gilmar Veloz alibainisha kuwa Chelsea walikuwa na nafasi ya kumsajili mteja wake huyo kwa mkataba wa miaka minne lakini klabu hiyo imeonekana kubadili uamuzi wake baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kuanza katika mbili pekee katika kipindi cha miezi minne walichokuwa naye.
No comments:
Post a Comment