Thursday, February 9, 2012
ADRIANO AFUNGIWA KWA AJILI YA DIET.
KLABU ya Corinthians ya Brazil imeamua kumfungia hotelini nyota wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Adriano na kumuamuru kula chakula maalumu na kufanya mazoezi ili kupunguza uzito na kurudi katika hali yake ya kawaida. Taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa mchezaji huyo atalazimika kubakia ndani ya hoteli hiyo katika makao makuu ya klabu hiyo mpaka mwishoni mwa wiki akiruhusiwa kula chakula atakachopewa na madaktari huku akitakiwa kufanya mazoezi mara tatu kwa siku. Mwalimu wa mazoezi wa klabu hiyo Fabio Mahseredjian wamefikia maamuzi ya kumfungia hotelini mchezaji huyo kwakuwa wameona ndio njia pekee ya kumzuia kula hovyohovyo kitu ambacho kinamuongeza uzito. Mahseredjian amesema mpishi wa timu hiyo anamtengenezea chakula pekee tofauti na wachezaji wenzake wa timu hiyo kwa Adriano mwenye umri wa miaka 29 ambacho atakuwa akipelekewa chumbani kwake.

No comments:
Post a Comment