Thursday, February 9, 2012
SUDAN KUSINI YAANZA HARAKATI ZA KUTAMBULIKA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA.
NCHI ya Sudan Kusini inatarajiwa kuwa mjumbe wa muda wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF ikiwa ni hatua moja ili ije kutambulika kama taifa jipya katika ulimwengu wa soka. Akizungumza kuhusu suala hilo Katibu Mkuu wa CAF Hicham El Amrani amesema kuwa nchi hiyo ambayo ilitengana na Sudan na kuwa taifa huru mwezi Julai mwaka jana itabidi isubiri miaka mingine miwili kabla ya kushiriki katika mishindano yote yanayoandaliwa na CAF. Nchi hiyo inatarajiwa kuzindua bendera yake katika sherehe zitazofanyika katika mkutano wa CAF jijini Libreville kesho na itaanza mara moja kupokea misaada kutoka shirikisho hilo kama nchi zingine. Chama kipya cha Soka cha Sudani ya Kusini kilianzishwa mwezi uliopita ambapo wanatarajiwa kufanya uchaguzi rasmi kuchagua viongozi wa chama hicho mwezi Aprili mwaka huu.

No comments:
Post a Comment