Thursday, February 9, 2012
REAL MADRID YAONGOZA ORODHA ZA KLABU TAJIRI DUNIANI.
KLABU za Real Madrid na Barcelona za Hispania ndizo klabu zinazoongoza kwa utajiri zaidi duniani katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo na kuna kuna dalili wakaendelea kuongoza katika kipindi kingine kirefu huko mbeleni. Katika ya orodha mwaka ilitolewa na Deloitte Madrid ndio wanaongoza katika orodha ya klabu zilizojikusanyia fedha nyingi zaidi kwa miaka saba mfululizo wakiwa wamejikusanyia pato la dola milioni 636.5 katika mwaka ulioishia June 30 pato hilo likiwa limepanda kwa asilimia tisa katika kipindi cha miezi 12. Mabingwa wa Uingereza Manchester United wenyewe wameshika nafasi ya tatu kwa mara nyingine wakiwa wamejikusanyia pato la dola milioni 487.2 ikiwa ndio timu inayoongoza kati ya timu nne za nchi hiyo zilizopo katika orodha ya 10 bora. Bayern Munich ya Ujerumani inashika nafasi ya nne ikiwa imejikusanyia pato linalofikia dola milioni 426.6 ikifuatiwa na Arsenal katika nafasi ya tano, Chelsea nafasi ya sita, AC Milan nafasi ya saba, Inter Milan nafasi ya nane, Liverpool nafasi ya tisa huku nafasi ya 10 ikishikwa na Schalke. Madrid ikiendelea kuongoza kwa mwingine mmoja itakuwa imefikia rekodi ya United ambao waliongoza orodha hiyo katika kipindi cha mwaka 1997 mpaka 2004 lakini wachambuzi wa mambo ya kiuchumi wanasema mafaniki inayopata uwanjani timu ya Barcelona inaweza kuongoza orodha hiyo mwaka ujao.

No comments:
Post a Comment