Tuesday, February 7, 2012

IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI TATU.

MSHAMBULIAJI wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic amefungiwa kucheza michezo mitatu kufuatia kumpiga mchezaji wa timu pinzani hivyo hawezi kuwemo katika kikosi cha timu hiyo kitapocheza mchezo muhimu wa Ligi Kuu nchini humo dhidi ya Juventus. Mchezaji huyo alitolewa dakika ya 64 wakati wa mchezo baina Milan dhidi ya Napoli Jumapili ambapo alimpiga kofi usoni beki wa Napoli Salvatore Aronica. Kwa kosa hilo alilofanya Ibrahimovic atakosa michezo migumu ya timu yake dhidi ya Udinese mwishoni mwa wiki hii mchezo dhidi ya Cesena ambao utachezwa wiki inayofuata na mchezo dhidi ya Juventus utakaochezwa Februari 25. Msimu huu Ibrahimovic ameisaidia timu yake hiyo ambayo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo akiwa amefunga mabao 15 ikiwa ni tofauti ya bao moja na Antonio Di Natale wa Udinese anayeongoza akiwa na mabao 16.

No comments:

Post a Comment