Tuesday, February 7, 2012
SAFA YAWAPIGA MARUFUKU MAWAKALA KUTEUA WAAMUZI WA MECHI ZA KIRAFIKI.
CHAMA cha Soka cha Afrika Kusini-SAFA kimeapa kutoruhusu mawakala kuteua waamuzi kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya kirafiki baada ya tuhuma za kupanga matokeo zilizotokea katika kipindi cha maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010. Gazeti moja nchini humo lilidai kuwa mechi baina ya Thailand, Bulgaria, Guatemala na Colombia zinaweza kuwa zilipangwa na Wilson Raj Perumal ambaye anatumikia miaka miwili jela nchini Finland baada ya kukumbwa na kashfa hiyo huko. Katika taarifa yake SAFA iliyotolewa Jumatatu imesema Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limewataka kutorusu mawakala kuteua waamuzi katika michezo ya kimataifa ya kirafiki ili kuepuka mambo hayo. Kwasasa FIFA ndio wanaoteua waamuzi wa kuchezesha michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia huku Shrikisho la Soka la Afrika-CAF lenyewe pia likiteua waamuzi kwa ajili michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Matifa ya Afrika hivyo kuziachia nchi wenyeji kuteua waamuzi kwa ajili ya michezo ya kirafiki.

No comments:
Post a Comment