Tuesday, February 7, 2012
BRADLEY KUENDELEA KUINOA MISRI.
KOCHA wa timu ya taifa ya Misri Bob Bradley amesema ataendelea kukinoa kikosi hicho pamoja na vurugu zilizotokea uwanjani na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70. Baada ya vurugu hizo zilizotokea Jumatano iliyopita katika mji wa Port Said Waziri Mkuu wa nchi hiyo aliwafukuza mara moja Rais wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-EFA na uongozi mzima wa chama hicho. Bradley ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Marekani amesema kuwa katika kipindi cha matatizo kama watu wanakiwa kuwa kitu kimoja na kuonyesha ujasiri na yeye akiwa kama kocha atajitahidi kufanya kila analoweza ili kuhakikisha anaisaidia timu hiyo. Kocha huyo hakuwa na uhakika wa mchezo wao wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 dhidi ya Afrika ya Kati ambao ulikuwa uchezwe Februari 29 mwaka huu kama utafanyika kutokana na vurugu zinaondelea mpaka hivi sasa.

No comments:
Post a Comment