Monday, February 6, 2012

KEITA AWAOMBA WANANCHI NCHINI KWAKE KUACHA MAPIGANO.

KIUNGO wa timu ya taifa ya Mali Seydou Keita amewaomba wananchi wa nchi hiyo kuacha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe akitumia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuombea amani. Zaidi ya watu 20 ambao ni waasi kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo wamekufa kufuatia mapigano ya siku mbili katika mkoa wa Timbuktu Jumamosi ambapo waasi hao wanadai sehemu hiyo itambuliwe kama nchi huru. Akihojiwa mara baada ya timu yake kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga Gabon kwa changamoto ya mikwaju ya penati Keita aliwaomba wananchi wa nchi hiyo kuacha mapigano na kuwa kitu kimoja kwakuwa wote wanatoka taifa moja. Mchezaji huyo pia alimuomba rais wa nchi hiyo kufanya kila awezalo kusimamisha mapigano hayo na kuongeza kuwa wana furaha kutinga hatua ya nusu fainali lakini muda huohuo wanajisikia vibaya kwa kile kinachoendelea nchini mwao.

No comments:

Post a Comment