Wednesday, February 8, 2012
SENEGAL YAMTIMUA TRAORE.
NCHI ya Senegal imemtimua kazi aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Amara Traore baada ya kikosi hicho kushindwa vibaya katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Kuondoka kwa kocha huyo ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa kikosi hicho kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia kulitangazwa Jumanne baada ya viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini lilipokutana jijini Dakar. Baada ya kufanya vizuri katika hatua ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano hiyo Senegal walikwenda Guinea ya Ikweta na Gabon ikiwa ni timu mojawapo inayopewa nafasi ya kufanya vizuri. Hatahivyo walipata mshangao wa kihistoria ya michuano hiyo baada ya kufungwa na Guinea ya Ikweta ambao wanashika nafasi ya 100 katika orodha za ubora duniani huku pia wakifungwa na Zambia na Libya na kuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo. Karim Sega na Aliou Cisse ndio wametajwa kukiongoza kikosi hicho katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Afrika Kusini-Bafana Bafana utakaochezwa Februari 29 jijini Durban.

No comments:
Post a Comment