ARSENAL YAKATA TAMAA NA VA PERSIE.
 |
| Robin van Persie. |
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Arsenal, Robin van Persie amerejea katika kambi ya mazoezi ya klabu yake hiyo jana na kuendelea kusisitiza kuwa bado anataka kuondoka. Klabu hiyo nayo inaonekana kukata tamaa na mchezaji huyo kwani katika orodha ya matangazo yake ya msimu ujao mchezaji huyo hajajumuishwa na wenzake. Mshambuliaji huyo ambaye ana thamani ya paundi milioni 30 anataka kufanya mazungumzo mapya na meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger na Ofisa Mkuu Ivan Gazidis juu ya mustakabali wake wa baadae. Msemaji wa klabu hiyo alithibisha uwepo wa mchezaji huyo katika kambi yao na kusema kuwa anataka kuzungumzia suala lake haraka iwezekanavyo lakini hakuna tarehe rasmi ya mkutano wa kukutana na nmchezaji huyo iliyopangwa mpaka sasa. Van Persie ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake anawindwa na vilabu mbalimbali kama Manchester City, Manchester United, Juventus na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment