Tuesday, July 17, 2012

BOLT ATAENDELEA KUWA RAFIKI YANGU HATA KAMA NIKIMSHINDA LONDON - BLAKE.

Usain Bolt.
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi Yohan Blake amesisitiza kuwa urafiki wa karibu ulipo kati yake na mwanariadha mwenzake Usain Bolt ambao wote wanatoka Jamaica utaendelea kudumu hata kama kukitokea chochote katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London, Uingereza. Blake amedhihirisha kuwa atakuwa tishio kwa Bolt katika kuwania medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 na 200 baada ya kufanikiwa kumshinda bingwa huyo wa olimpiki katika mbio zote hizo katika mashindano ya majaribio yaliyofanyika Jamaica. Kiwango alichokionyesha Blake katika mashindano ya Kingston mwishoni mwa Juni kimeonyesha kuwa mwanariadha huyo atakuwa tishio kwa Bolt jijini London lakini mwenyewe anamsema kuwa kama akishinda, akishindwa au hata kumaliza mbio hizo wakiwa sawa urafiki wao utaendelea palepale. Blake alifanikiwa kutawala mashindano ya dunia yam bio za mita 100 zilizofanyika Daegu mwaka jana akitumia muda wa sekunde 9.92 ingawa hata hivyo alishinda medali hiyo baada ya Bolt kuenguliwa kwenye fainali yam bio hizo baada ya kuanza kukimbia kabla ya wenzake. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya mbio fupi na Blake wanafundishwa na mwalimu mmoja ambapo muda mwingi wamekuwa wakifanya mazoezi pamoja.

No comments:

Post a Comment