BIN HAMMAM ATAMANI KUSTAAFU MASUALA YA SOKA KUTOKANA NA KUONEWA WIVU.
 |
| Mohammed bin Hammam. |
MGOMBEA urais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA, Mohammed bin Hammam ambaye kifungo chake cha maisha kujishughulisha na masuala ya michezo kilitenguliwa na Makahama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS amesema kuwa nataka kustaafu masuala ya michezo. Bin Hammam mwenye miaka 63 ambaye alikuwa anatuhumiwa kuwahonga rushwa ya fedha wajumbe wa FIFA ili wampigie kura wakati wa kampeni za urais wa shirikisho hilo mwaka uliopita amesema kuwa anataka kuachana na masuala ya soka kutokana na kile alichokiita wivu katika mchezo wa soka. Mapema wiki hii Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar alisimamishwa kwa siku 30 nafasi yake kama rais wa Shirikisho la Soka barani Asia-AFC ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mpya za rushwa zinazomkabili kwenye shirikisho hilo. Akihojiwa na shirikika la habari la BBC, Bin Hammam amesema kuwa anatamani kustaafu kuwa kiongozi wa soka baada ya kutumikia kwa karibu miaka 42 kutokana na wivu waliokuwa nao wapinzani wake katika soka. Maofisa wa AFC hawakupatikana mara moja kuzungumzia kauli hiyo ya kiongozi wao wakati Peter Velappan ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa AFC kwa kipindi cha miaka 30 na mpinzani mkubwa wa Bin Hammam alikataa kuzungumza lolote kuhusiana na suala hilo.
No comments:
Post a Comment