Saturday, July 21, 2012

CASSANO APIGWA FAINI NA UEFA KWA KUPONDA MASHOGA.

Antonio Cassano.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Italia, Antonio Cassano ametozwa faini kutokana na kauli aliyotoa kuhusiana na suala ushoga kwa wachezaji kwenye michuano ya Ulaya iliyomalizika mapema mwezi huu. Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA limemtoza mchezaji huyo kiasi cha dola 18,000 kutokana na kauli yake hiyo aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari nchini Poland mwezi uliopita. Cassano alikaririwa akiswema kuwa ana matumaini hakuna mchezaji anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja katika timu ya taifa ya nchi hiyo na baadae kutumia neon la kudhalilisha watu wenye tabia kama hizo. Cassano anaweza kukata rufani kutokana na uamuzi huo uliotolewa na UEFA.

No comments:

Post a Comment