DILI LA IBRAHIMOVIC KWENDA PSG LAKAMILIKA.
 |
| Zlatan Ibrahimovic. |
MSHAMBULIAJI wa klabu ya AC Milan ya Italia, Zlatan Ibrahimovic amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ya Ufaransa. Wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola amekuwa katika mazungumzo na PSG kwa siku kadhaa na kutangaza jana kwa wamefikia makubaliano ya uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden. Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo alithibitisha suala ana akusema kuwa mchezaji anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na kama kila kitu kikienda sawa atasaini mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo. Usajili huo wa Ibrahimovic utakuwa wa tatu kwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 baada ya pia kumsajili Thiago Silva naye kutoka AC Milan na Ezequiel Lavezzi kutoka Napoli.
No comments:
Post a Comment