Thursday, July 19, 2012
KHAN ATAKA KURUDIANA NA GARCIA DESEMBA.
BONDIA Amir Khan wa Uingereza anatarajiwa kurejea ulingoni Desemba mwaka huu kwa ajili ya pambano la marudiano dhidi ya Danny Garcia pamoja na bondia huyo kutoka Marekani kukataa kurudiana na Muingereza huyo. Khan alipata kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa Garcia kwa kumpiga katika raundi ya nne ya pambano hilo la raundi 12 lililofanyika jijini Las Vegas, Marekani Jumapili iliyopita. Akihojiwa Khana amesema kuwa kuwa anategemea kurejea ulingoni mapema iwezekanavyo lengo kubwa likiwa ni kutetea mkanda wake wa WBA ambao aliupoteza kwa Garcia wakati walipopambana. Hilo linakuwa ni pambano la tatu kwa Khan toka aingie katika ulimwengu wa masumbwi pambano la kwanza kupigwa likiwa lile alilopambana dhidi ya Breidis Prescott katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini Athens mwaka 2008 na linguine alilopigwa na Lamont Peterson Desemba mwaka jana.

No comments:
Post a Comment