Thursday, July 19, 2012

UINGEREZA YAPOTEZA KWA MAREKANI KIKAPU.

KOMBAINI ya timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Uingereza imefungwa na Marekani vikapu 88-63 katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya michuano ya Olimpiki ambayo inarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. Uingereza ilianza vyema mchezo huo na kuwapa tabu Marekani ambao ni mabingwa mara sita wa michuano ya olimpiki kutokana na kujilinda vyema na kuwanyima nafasi ya kufunga wapinzani wao. Lakini kutokana na uzoefu wa marekani ambao wachezaji wake wengi wanacheza katika ligi ya kikapu ya NBA walifanikiwa kuwaonyesha Uingereza uzoefu wao kwa kuwasambaratisha kwa vikapu hivyo kwenye mchezo uliofanyika jijini Manchester. Uingereza waliwashangaza Marekani baada ya kwenda mapumziko katika robo ya kwanza wakiwa wanaongoza kwa vikapu 15-8 lakini Marekani ilizinduka katika robo ya pili na kufanikiwa kuongoza kwa 47-32. Toka hapo Marekani ambayo ilikuwa ikiwatumia wachezaji wake nyota wazoefu kama Maya Moore ambaye alifunga vikapu 18 katika mchezo huo waliendelea kutawala mchezo mpaka unamalizika kwa kuibuka kidedea.

No comments:

Post a Comment