ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Habari wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF, Suleiman Habuba ameamua kujiuzulu wadhfa wake huo na kuangalia changamoto nyingine. Habari za kujiuzulu kwa Habuba zimekuwa za kustusha haswa ukizingatia maendeleo yaliyofikiwa katika kitengo cha habari cha CAF katika kipindi chake wakati akiwa kiongozi. Habuba alithibisha habari hizo za kuachia wadhfa huo akiwa katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri ambapo alijiunga na CAF na kupewa kitengo hicho cha habari mwaka 2003. Akihojiwa mara baada ya uamuzi huo Habuba amesema kuwa imekuwa ni heshima kwake kufanya kazi na shiirikisho hilo katika kipindi cha miaka tisa ambayo imekuwa ya mafanikio katika kazi yake na maisha yake kwa ujumla. Kwasasa kaimu katibu mkuu wa CAF, Essam Ahmed ndiye ameteuliwa kushika wadhfa huo kwa muda kama mkurugenzi wa habari.
Sunday, July 22, 2012
MKURUGENZI WA HABARI CAF AJIUZULU.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment