Sunday, July 22, 2012

MUAMBA AKIMBIZA MWENGE WA OLIMPIKI.

Fabrice Muamba.
KIUNGO wa klabu ya Bolton Wanderers, Fabrice Muamba amekimbiza mwenge wa Olimpiki katika mitaa ya jiji la London ikiwa ni miezi mine toka alipoanguka uwanjani na kupoteza fahamu katika mchezao wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Moyo wa Muamba ulisimama kufanya kazi kwa muda wa dakika 78 Machi 27 mwaka huu baada ya kuanguka wakati wa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspurs. Wakati ambapo bado hajapona vizuri kurejea dimbani, Muamba aliweza kutembea mita 300 akiwa na mwenge huo jana wakati ulipotua katika jiji hilo ambalo ndio watakuwa wenyeji wa michuano hiyo. Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiye alikuwa mkimbizaji wa mwisho wa mwenge huo katika mji wa Walthamstow ambao alikuja kuishi mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 11 baada familia yake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe huko kwao. Mwenge huo ambao tayari umeshatembea maeneo mbalimbali nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 60 utaendelea na ziara yake katika mitaa ya London mpaka safari yake ya mwisho ambayo itakuwa katika Uwanja wa Olimpiki kwenye sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo Ijumaa.

No comments:

Post a Comment