BABU YAKE ROSSI AMSEMEA MBOVU PRANDELLI KWA KUMUACHA MJUKUU WAKE KATIKA KIKOSI CHA ITALIA.

BABU wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Fiorentina, Giuseppe Rossi amemshutumu kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli kwa kumuita msaliti baada ya kocha huyo kumuengua mchezaji huyo katika kikosi chake cha Kombe la Dunia. Mshambuliaji huyo ndio alikuwa amepona majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa miezi na kujumuishwa katika kikosi cha Italia kilichotoa sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland iliyochezwa Jumamosi iliyopita. Lakini Prandelli ambaye alikiri mchezo huo ulikuwa muhimu kuelekea kuteua kikosi chake cha mwisho kwa ajili ya michuano hiyo ya Brazil alimuengua nyota huyo mzaliwa wa Marekani ambaye hiyo itakuwa michuano yake ya tatu mfululizo ya kimataifa kuikosa. Babu yake Rossi, aitwaye Bruno Petrocelli alionyesha hasira zake za wazi wakati akihojiwa katika radio moja nchini Italia akidai kuwa kocha huyo amekuwa kama msaliti kutokana na maneno mazuri aliyokuwa akiyazungumza hapo mwanzo. Petrocelli amesema haoni sababu haswa ya Prendelli kumuacha mjukuu wake huyo katika kikosi chake haswa ikizingatiwa kuwa hivi yuko fiti kabisa kiafya.
No comments:
Post a Comment