KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza, Frank Lampard anafikiria kuhamia katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS baada ya kuondoka Chelsea. Lakini nyota huyo amesema hatatoa maamuzi yoyote mpaka baada ya kumaliza michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil akiwa na timu yake ya taifa. Lampard mwenye umri wa miaka 35 alitangaza kuondoka Stamford Bridge baada ya kucheza hapo kwa miaka 13 Jumatatu wiki hii na amekuwa akiwindwa na klabu ya New York City FC ambayo ni mpya katika ligi hiyo. Akihojiwa Lampard amesema Marekani inaweza kuwa chaguo lake ingawa bado anaangalia na sehemu zingine tofauti lakini bado anataka kuendelea kucheza soka. Kiungo huyo wa zamani wa West Ham United atakuwa amecheza mechi 104 za kimataifa wakati atakapoingoza Uingereza kama nahodha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ecuador baadae leo.

No comments:
Post a Comment