KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata amebainisha kuwa amefikia makubaliano na klabu ya Difaa Hassani d'El Jadida ya Morocco kwa ajili ya kuifundisha msimu ujao. Difaa ilishindwa kumuongeza mkataba kocha wake Abdelhak Benchikha raia wa Algeria ambaye amechukuliwa na mahasimu wao Raja Casablanca. Shehata aliuambia mtandao wa Supersport kuwa tayari wameshafikia makubaliano ya kuingoza timu hiyo kwa misimu miwili na anachisubiri ni mwenyekiti wa Difaa kwenda jijini Cairo kwa ajili ya kusaini mkataba na baadae kuutangaza. Taarifa zimekuja sambamba na taarifa zingine kutoka katika vyombo vya habari kutoka Misri vilivyodai anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa Zamalek ambayo imetimua kocha wake wa sasa Ahmed Hossam Mido mwishoni mwa msimu huu. Baada ya kuondoka Zamalek mwaka 2012, Shehata mwenye umri wa miaka 64 alikwenda kuifundish Al Arabi ya Qatar kwa miezi michache kabla ya kujiuzulu wadhfa wake huo.

No comments:
Post a Comment