Monday, June 9, 2014

HISPANIA WANATUHESHIMU - MARCELO.

BEKI wa klabu ya Real Madrid, Marcelo anaamini siku zote Hispania wamekuwa na heshima kwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, Brazil. Beki huyo wa kushoto alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kiliwasambaratisha mabingwa hao wa Ulaya na Dunia Hispania katika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa mwaka jana katika ardhi yao. Na Marcelo amebainisha kuwa kufuatia ushindi huo, wachezaji wa Hispania walikipongeza kikosi cha Brazil kwa kiwango bora walichoonyesha katika mchezo huo. Marcelo amesema anajua Hispania wanaiheshimu Brazil kwasababu alifanya mazungumzo na Iker Casillas baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho na alimwambia kuwa kwa ushindi huo waliopata ndio maana nchi hiyo siku zote imekuwa ikiheshimika. Beki aliendelea kudai kuwa anajua msukumo utakuwa mkubwa lakini hana shaka kwasababu siku zote mashabiki wao wamekuwa pamoja nao na huwasaidia katika kipindi kigumu.

No comments:

Post a Comment