SHIRIKA la kutoa huduma za kibinadamu la Oxfam limeendesha kile inachosema kuwa Kombe la Dunia Mbadala ili kuona jinsi gani pengo la matajiri na masikini linavyozidi kuwa kubwa katika nchi zinazoshiriki michuano hiyo kwa mwaka huu. Katika kinyang’anyiro hicho Ubelgiji ndio wametangazwa washindi kutokana na mwanya wa matajiri na masikini kuwa mdogo katika nchi hiyo. Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, Brazil wao wameshindwa kufuzu hata mzungumko wa pili kutokana na jinsi pengo la matajiri na masikini lilivyokuwa kubwa miongoni mwa wananchi wake. Mataifa mengineyo ya America Kusini pia hayajafanya vizuri lakini inasemekana yanajitahidi, huku cha ajabu mataifa ya kiafrika yanayoshirki Kombe la Dunia hayajatajwa.

No comments:
Post a Comment