KIUNGO mahiri Andrea Pirlo ameipa Juventus ahueni baada ya kukubalia kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 kwasasa yupo na timu ya taifa ya Italia katika michuano ya Kombe la Dunia lakini amefikia makubaliano ya kuendelea kubakia kwa mabingwa hao wa Serie A mpaka mwaka 2016. Pirlo alitua Juventus Mei mwaka 2011 baada ya kuachwa na klabu ya AC Milan na kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Serie A katika kila msimu toka alipofika. Mbali na kushinda mataji hayo pia ameshinda mengine mawili ya Kombe la Italia katika mechi zake 131 alizoichezea timu hiyo mpaka sasa.

No comments:
Post a Comment